Indirimbo Zikundwa Open in the app

#15

Mungu unitume, Moto wako sasa

Wokovu

Couplet 1

Mungu, unitume Moto wako sasa, Ninangoja nguvu yako! Nipe na uzima na upendo wako, unijaze, e’ Mwokozi wangu!

Couplet 2

Teketeza yote usiyoyapenda, nisafishe kati’ Damu! Na kiburi changu ukivunje tena, unioshe, Yesu, niwe safi!

Couplet 3

Unilinde, Yesu, sikuasi tena, unifunge kwa upendo! Mimi ni dhaifu, unitunze kwako, ’niongoze kwa mkono wako!

Couplet 4

Huko juu kwako tutaona raha, na huzuni itakwisha. Nyimbo za shukrani zitajaza Mbingu: utukuzwe Yesu Mkombozi.