Indirimbo Zikundwa Open in the app

#17

Ukae nami, giza inafika

Wokovu

Couplet 1

Ukae nami, giza inafika! Usiniache, Mungu nakuomba! Unayejua udhaifu wangu, nategemea wewe, ’kae nami!

Couplet 2

Maisha yangu ni mafupi sana, uzuri wa dunia utakwisha. Kuna machozi, kufa huku chini, wewe Mwokozi wangu ’kae nami!

Couplet 3

Nakuitaji wewe siku zote, unaweza sana kunilinda. Wewe shujaa wakushinda wote. Katika hali zote ’kae nami!

Couplet 4

Unionyeshe Msalaba wako, nione nuru yako kati’ giza! Na nikiishi au nitakufa. Wewe, Mwokozi wangu ’kae nami!