Indirimbo Zikundwa Open in the app

#14

Mwokozi wangu ulikwenda juu

Wokovu

Couplet 1

Mwokozi wangu ulikwenda juu kukaa kuumeni kwake Baba; Utakusanya sisi sote huko, Mbinguni kwako, utatufikishsa. :/: Makao mema wa’tuandalia, unatungoja kwake Mungu Baba. :/:

Couplet 2

Mwombezi wetu wewe, Yesu Kristo, kwa’jili yetu mbele yake Baba. Wachunga sana sisi, kundi lako, na watusaidia ’jaribuni. :/: Na siku zote unatuombea, watushindia vita kali huku. :/:

Couplet 3

Mikono yako uliwanyoshea walio wako, siku uli’kwenda; na hivyo siku utakaporudi utabariki wakuaminio. :/: Ulivyokwenda, utakavyorudi; niombe nikakeshe kwa imani!. :/: