#6
Twa’sifu Mungu kwa ajili ya Damu
Wokovu
Couplet 1
Twa’sifu Mungu kwa ajili ya Damu takatifu, Inayotosha, kuondoa makosa yetu yote.
Couplet 2
Wakristo wanakusanyika karibu ya kisima, hawapungukiwi kitu, wakaa kwa Mwokozi.
Couplet 3
Tuimbe duniani pote juu ya Pendo kubwa, kwa kuwa tumefunguliwa kisima cha Golgotha.
Couplet 4
Kisima hicho, Yesu Kristo, na Damu yake: Damu yake. Wasumbukao wastarehe, waburudishwe hapa.
Couplet 5
Na wenye dhambi wanaitwa kwa wingi wa rehema, na wakosaji na maskini wasaidiwa sana.
Couplet 6
Tumeipata tunu kubwa, Neema kwa neema, apokeaye fungu lake ni mtu wa uheri.
Couplet 7
Haleluya! Tuna’himidi Mwenyezi na Mwanawe na Roho ’takatifu pia. Haleluya! Amina.