Indirimbo Zikundwa Open in the app

#7

Mwokozi ameutimiza Wokovu

Wokovu

Couplet 1

Mwokozi ameutimiza Wokovu Kwa Neema kubwa, na juu ya Mwamba wa neno la Mungu najenga imani.

Refrain

Aliniokoa kabisa. Kwa Damu alinisafisha. Ninamshukuru Mwokozi kwa sababu alinikomboa hakika!

Couplet 2

Mzigo wa dhambi aliuondoa kwa Neema kubwa. Naona furaha rohoni kabisa, Amani yangu.

Refrain

Aliniokoa kabisa. Kwa Damu alinisafisha. Ninamshukuru Mwokozi kwa sababu alinikomboa hakika!

Couplet 3

Naweza kukaa mweupe rohoni kwa Neema kubwa; na Roho ya Mungu inaniongoza njiani daima.

Refrain

Aliniokoa kabisa. Kwa Damu alinisafisha. Ninamshukuru Mwokozi kwa sababu alinikomboa hakika!

Couplet 4

Karibu na Yesu nalindwa salama kwa Neema kubwa. Ahadi za Mungu zanipa furaha iliyo kamili.