Indirimbo Zikundwa Open in the app

#5

Dhahabu na fedha haziniokoi

Wokovu

Couplet 1

Dhahabu na fedha haziniokoi, Hazina na mali haziponyi roho, Lakini kwa Damu ya Yesu Mwokozi Nime nunuliwa nipate uhuru.

Refrain

Nakombolewa pasipo mali, kwa Neema nimeokoka! Ni bei ghali: kwa Damu yake alilipa deni langu.

Couplet 2

Dhahabu na fedha hazinilipii madeni makubwa ninayo kwa Mungu. Mwokozi alinikomboa kwa Damu. Nipate Wokovu nitoke dhambini.

Refrain

Nakombolewa pasipo mali, kwa Neema nimeokoka! Ni bei ghali: kwa Damu yake alilipa deni langu.

Couplet 3

Dhahabu na fedha haziufungui Mlango waku’karibia Mwokozi, Lakini kwa Damu nimeifikia Neema ya Mungu aliye mkuu.

Refrain

Nakombolewa pasipo mali, kwa Neema nimeokoka! Ni bei ghali: kwa Damu yake alilipa deni langu.

Couplet 4

Dhahabu na fedha hazinifikishi Nyumbani mwa Mungu nilie mwasia, Lakini nimekombolewa kwa Damu, Kwa hiyo nitachukuliwa Mbinguni.

Refrain

Nakombolewa pasipo mali, kwa Neema nimeokoka! Ni bei ghali: kwa Damu yake alilipa deni langu.