Indirimbo Zikundwa Open in the app

#4

Usiku kabla ya kuteswa Yesu

Wokovu

Couplet 1

Usiku kabla yakuteswa, Yesu Alikusanya wanafunzi wake; Alifahamu kwamba saa yake Yakutolewa ilikaribia.

Couplet 2

Kwa roho aliona Gethsemane, Maneno yake na huzuni nyingi; Zaidi aliofu saa ile, ata’poachwa hata naye Mungu.

Couplet 3

Alitamani saa ya pasaka Pamoja na wapendwa wake huku. Katika pendo lake kubwa sana Aliyashinda majaribu yote.

Couplet 4

Akautwa’ mkate aka’mega, ’Twaeni, mle, huu ni mwili wangu! Na akawapa wanafunzi wake. Wa heri kila mtu ’aminiye.

Couplet 5

Ba’daye akawapa na kikombe, Na akasema: «Nyweni nyote hiki! Ni Damu yangu inayo mwangika Kwa ondoleo la makosa yote.