Indirimbo Zikundwa Open in the app

#3

Kisima safi sana chatoka Msalaba

Wokovu

Couplet 1

Kisima safi sana chatoka Msalaba, Kimetufungukia, chasafisha vema. Twaweza kusikia sauti yake Yesu: «Unifuate sasa kwa kiti cha neema».

Refrain

Kisima cha Msalaba, Damu ya Yesu Kristo, chatusafisha sisi sote na dhambi na uchafu.

Couplet 2

Ufike, mwenye dhambi, kisima ni karibu. Uache dhambi zako, upumzike hapa! Katika Damu yake kabisa utapona, Tazama Msalaba, kisima kitokako!

Refrain

Kisima cha Msalaba, Damu ya Yesu Kristo, chatusafisha sisi sote na dhambi na uchafu.

Couplet 3

Kisima hicho safi cha Damu ya Mwokozi. Kinatutia afya na nguvu ya kushinda. Mfalme wetu, Yesu, tumhimidi tena! Furaha yetu yote ni kushukuru Mungu!

Refrain

Kisima cha Msalaba, Damu ya Yesu Kristo, chatusafisha sisi sote na dhambi na uchafu.