#2
Kijito kiko chenye Damu
Wokovu
Couplet 1
Kijito kiko chenye Damu itokayo Mwokozi. Kiwaoshacho wakosaji :/: Na dhambi na uchafu. :/:
Couplet 2
Msalabani mnyang’anyi alikiona hima. Mnyonge mimi kama yeye :/: Nitakasike pia. :/:
Couplet 3
Mwokozi wetu, Damu yako daima ina nguvu. Ya kuokoa wenye dhambi :/: Wa makabila yote. :/:
Couplet 4
Kijito hicho cha ajabu ni tumaini langu. Upendo wako nausifu, :/: Nausifu hata kufa. :/:
Couplet 5
Nimeamini, naamini uliye nifilia, Msalabani umetoa :/: Maisha yako Yesu. :/: