#1
E Yesu Mshindaji wa Golgotha
Wokovu
Couplet 1
E Yesu Mshindaji wa Golgotha, twakusifu! Bendera ya mapenzi ni alama ya kushinda. Ulichukuwa dhambi zetu juu ya Msalaba wako. Twakuhimidi, Bwana na Mfalme! Haleluya!
Couplet 2
Twashinda na zaidi ya kushinda kati’ yote. Kwa Damu yako, Yesu, na watuinua moyo. Katika vita na ’jaribu twaipeleka kwa furaha Bendera yako nzuri ya kushinda kati’ vita.
Couplet 3
Mbinguni Mkombozi ni Mkuu mwenye sifa. Aliondoa dhambi kwa kutufilia wote. Mwana Kondoo wake Mungu, Umestahili kupokea Uweza, Utukufu na Heshima. Haleluya!