#574
Cha kutumaini sina
Umuco 2
Couplet 1
Cha kutumaini sina, Ila Damu yake Bwana, Sina wema wa kutosha, Dhambi zangu kuziosha.
Refrain
Kwake Yesu nasimama, Ndiye Mwamba: Ni Salama, Ndiye Mwamba: Ni Salama, Ndiye Mwamba: Ni Salama.
Couplet 2
Njia yangu iwe ndefu, Yeye hunipa Wokovu, Mawimbi yakinipiga, Nguvu zake ndiye nanga.
Refrain
Kwake Yesu nasimama, Ndiye Mwamba: Ni Salama, Ndiye Mwamba: Ni Salama, Ndiye Mwamba: Ni Salama.
Couplet 3
Damu yake na Sadaka, Nategemea daima, Yote chini yakiisha, Mwokozi Atanitosha.
Refrain
Kwake Yesu nasimama, Ndiye Mwamba: Ni Salama, Ndiye Mwamba: Ni Salama, Ndiye Mwamba: Ni Salama.
Couplet 4
Nikiitwa Hukumuni, Rohoni nina Amani, Nikivikwa Haki Yake, Sina hofu mbele Zake.