Indirimbo Zikundwa Open in the app

#543

Mara ngapi ulinivumilia?

Umuco 2

Couplet 1

Mara ngapi ulinivumilia Bwana Mungu, Kama mzazi kwa mtoto wake mpendwa? Kiisha ukanyoosha mkono wako wa uwezo, Nikapata kufikilia Wokovu wako.

Refrain

Neema... Rehema zako Bwana, Nini kama Neema ya Bwana Mungu? Neema... rehema zako Yesu, Ninajisifia Neema hiyo, Ninajisifia Neema.

Couplet 2

Dhambi gani sikukutendea mimi muovu? Alakini kati mambo yote huku chini, Kwa jicho lako haukuniachilia kamwe, Hadi siku kuu hiyo ya Wokovu wangu.

Refrain

Neema... Rehema zako Bwana, Nini kama Neema ya Bwana Mungu? Neema... rehema zako Yesu, Ninajisifia Neema hiyo, Ninajisifia Neema.

Couplet 3

Kumbe nilikuasi bila kufahamu, Bwana, Kwa kupenda dunia na maovu yake Ningelijua kwamba Neno ndiye Baba Mungu... Ningelibaki nyuma yako kama Elisha.

Refrain

Neema... Rehema zako Bwana, Nini kama Neema ya Bwana Mungu? Neema... rehema zako Yesu, Ninajisifia Neema hiyo, Ninajisifia Neema.

Couplet 4

Kama yule nguruwe nilirudi duniani, Kula na kujivuruga ndani matapishi Na sikujali damu yako Bwana wangu Yesu... Bwana, samehe upumbavu wa mtu bure!

Refrain

Neema... Rehema zako Bwana, Nini kama Neema ya Bwana Mungu? Neema... rehema zako Yesu, Ninajisifia Neema hiyo, Ninajisifia Neema.

Couplet 5

Badae nilijiona kuwa mwenye fahamu, Lakini sikuweza kufikiria kwamba mwisho wa akili yangu ndio mwanzo wa Hekima Yako Mungu muumba wa mbingu na dunia.

Refrain

Neema... Rehema zako Bwana, Nini kama Neema ya Bwana Mungu? Neema... rehema zako Yesu, Ninajisifia Neema hiyo, Ninajisifia Neema.

Couplet 6

Niliposhuhudia nyumbani mwa Baba yangu, Nilitubu na kukiri “Yesu ndiye Bwana” Sababu sikustahili kati watakatifu, Ndipo niliomba basi nafasi ya mwisho.

Refrain

Neema... Rehema zako Bwana, Nini kama Neema ya Bwana Mungu? Neema... rehema zako Yesu, Ninajisifia Neema hiyo, Ninajisifia Neema.

Couplet 7

Kisha nilipogeuka na kutazama nyuma Nilililia neema yako nikisema: “Nikamate mkono kwa uwezo wako Baba, Ili nisirudi tena kucheza na kifo!”

Refrain

Neema... Rehema zako Bwana, Nini kama Neema ya Bwana Mungu? Neema... rehema zako Yesu, Ninajisifia Neema hiyo, Ninajisifia Neema.

Couplet 8

Nilipofika kwenye msalaba wako Kristo, Ndipo niliona Upendo wako halisi, Roho ikapata neema na rehema zako, Hakika ndio upendo wa Yesu Mwokozi.

Refrain

Neema... Rehema zako Bwana, Nini kama Neema ya Bwana Mungu? Neema... rehema zako Yesu, Ninajisifia Neema hiyo, Ninajisifia Neema.

Couplet 9

Kwa muda kitambo, ndipo niliona upendo, Ukimeza mashaka niliokuwa nayo, Nikajikuta kati ya watakatifu wako Shukurani na sifa viwe vyako daima!

Refrain

Neema... Rehema zako Bwana, Nini kama Neema ya Bwana Mungu? Neema... rehema zako Yesu, Ninajisifia Neema hiyo, Ninajisifia Neema.

Couplet 10

Nikikumbuka siku ile ya Wokovu wangu, Moyo huwaka kabisa moto wa uzima, Ahadi zako ninanishikilia hakika, Tumaini langu ni: uzima wa milele.