#514
Wakati wa nuhu
Umuco 2
Couplet 1
Wakati wa Nuhu watu walimuasi Mungu, wengi walitenda kila dhambi. Walimchukiza Mungu kwa dhambi zao nyingi, kwa kumuasi Muumba.
Refrain
Mungu alimwambia Nuhu kujenga safina, kwa dhambi zao nyingi walifunganiwa; Nasi tuwe imara tusifunganiwe.
Couplet 2
Nuhu alikuwa akisema wakimcheka, wakifikiri ni upuuzi. Hawakuweza kutii Neno lake Mungu, walikufuru kwa Neno.
Refrain
Mungu alimwambia Nuhu kujenga safina, kwa dhambi zao nyingi walifunganiwa; Nasi tuwe imara tusifunganiwe.
Couplet 3
Mungu alimwambia Nuhu kujenga safina, na kuingia na jamii yake. Walioingia wote pamoja na Nuhu, ndio walinusurika.
Refrain
Mungu alimwambia Nuhu kujenga safina, kwa dhambi zao nyingi walifunganiwa; Nasi tuwe imara tusifunganiwe.
Couplet 4
Mvua nyingi ilinyesha bila kukatika, maji yalizidi kuongezeka. Walianza kukumbuka maneno ya Nuhu, kuhusu Neno la Mungu.
Refrain
Mungu alimwambia Nuhu kujenga safina, kwa dhambi zao nyingi walifunganiwa; Nasi tuwe imara tusifunganiwe.
Couplet 5
Walipanda kwenye milima hawakupona, wengine kupanda juu ya miti, wengine waligonga sana kwenye safina: ‘‘Nuhu fungua mlango’’.
Refrain
Mungu alimwambia Nuhu kujenga safina, kwa dhambi zao nyingi walifunganiwa; Nasi tuwe imara tusifunganiwe.
Couplet 6
Ndugu jichunguze kama waona safina, huyu ndiyo wakati wa Nuhu. Muda kitambo Mungu Atafunga mlango, usije ukachelewa.