#513
Sisi waheri wake bwana
Umuco 2
Couplet 1
Sisi waheri wake Bwana Yesu, Tuishi tu kwa kumtegemea. Aliyemtegemea Mwokozi wetu, hatapatwa na shida kamwe.
Couplet 2
Shida na jaribu kwa walio waheri, huwaletea amani na raha. Kwa kuwa Uheri wa Bwana Yesu, kwao tu ndio wanaoutegemea.
Couplet 3
Kwa kitambo tu hapa duniani, Tujiweke watakatifu kwake Mwokozi, maishani mwetu hapa duniani, Tuonekane kama Washindaji.
Couplet 4
Neno lake Mwokozi wetu Yesu, ndilo tu laweza kutuongoza maishani mwetu kitambo hapa, mpaka tupandishwe kwake Mbinguni.
Couplet 5
Tufurahi sana myoyoni mwetu, kwa Ukweli wake Aliotufunulia. Myoyoni mwetu tuimbe kwa shangwe, kwa Neema hizo zake Mwokozi.
Couplet 6
Ushukuriwe Mwokozi wetu Yesu, myoyoni mwetu twakuimbia kwa shangwe, Utusaidiye duniani hapa, tuishi tu kwa kukutegemea.