Indirimbo Zikundwa Open in the app

#162

Tunakimbilia uzuri wako

Umuco

Couplet 1

Tunakimbila uzuri wako Bwana wangu, sawa ndege amkiavyo asubuhi, twapaza sauti yetu tukisema, Mungu wetu tusikilize daima.

Refrain

Moyo hunyenyekea, O’Mungu wangu, nitakuimbia kwa sauti yangu yote ./.Huo ndio uzima wangu./.

Couplet 2

Tunakimbilia utukufu wako Baba Mungu, shabaa yetu tunataka kufanana nawe, tunakimbilia uso wako Baba Mungu, utujalie utujaze nguvu zako.

Refrain

Moyo hunyenyekea, O’Mungu wangu, nitakuimbia kwa sauti yangu yote ./.Huo ndio uzima wangu./.

Couplet 3

Tunakimbilia mikono yako Bwana Mungu, tushike mikono tusije tukatereze, tunakuletea unyonge wetu Bwana Mungu, utujalie utujaze nguvu zako.

Refrain

Moyo hunyenyekea, O’Mungu wangu, nitakuimbia kwa sauti yangu yote ./.Huo ndio uzima wangu./.

Couplet 4

Tunakuletea upumbavu wetu Bwana Mungu, utujalie utujaze hekima yako, tunakuleteya kiburi chetu Bwana Yesu, utujaze unyenyekevu wako.

Refrain

Moyo hunyenyekea, O’Mungu wangu, nitakuimbia kwa sauti yangu yote ./.Huo ndio uzima wangu./.

Couplet 5

Furaha gani kukuona kati yetu Bwana, ni kama nyumba ilio na mwamba, furaha gani kukuona ndani yetu Bwana, ni furaha na raha zaidi.

Refrain

Moyo hunyenyekea, O’Mungu wangu, nitakuimbia kwa sauti yangu yote ./.Huo ndio uzima wangu./.