#114
Ulitoka huko misri
Umuco
Couplet 1
Ulitoka huko misri, bondeni mwa uovu, ukavuka bahari nyekundu, ukakua wa Yesu, Mungu akakuvukisha bahari nyekundu, ukaanza safari, ya kwenda Sayuni uwe tayari katika safari.
Refrain
./.Jiepushe na kiburi, Jiepushe na mwili, jiepushe na hakili, jiepushe na uvivu, jiepushe na ujuwaji; ambatana na hekima utakua mwenye’heri siku zote./.
Couplet 2
Uliona nguzo ya moto, uliona manu kushuka, mwamba nao ukapasuka, na wa falme wakashindwa, uliona mambo mengi katika jangwa, iyo haitoshi ambatana na Yosua usije ukafia jangwani.
Refrain
./.Jiepushe na kiburi, Jiepushe na mwili, jiepushe na hakili, jiepushe na uvivu, jiepushe na ujuwaji; ambatana na hekima utakua mwenye’heri siku zote./.
Couplet 3
Uliona nguvu za Mungu, katika vyote uwazi, unajua njia za Mungu, na mapito yake yote, lakini haitoshi, zidisha kumuona, wengi katika Israeli wameona yote, lakini wameishia jangwani.
Refrain
./.Jiepushe na kiburi, Jiepushe na mwili, jiepushe na hakili, jiepushe na uvivu, jiepushe na ujuwaji; ambatana na hekima utakua mwenye’heri siku zote./.
Couplet 4
Waweza kuwa katika taifa hilo la ajabu, lakini wewe kama haukwi kama Kalebu, na wewe utaishia jangwani ndugu, usichokee ndani ya wokovu. Jiepushe ujuaji wako.