Indirimbo Zikundwa Open in the app

#390

Mateso ya muda kitambo

Umuco 1

Couplet 1

Tujiweke tayari kwa Bwana, Tuendee kwa Neno, Ndipo tutapata kumpendeza, Tukaende Mbinguni (kwake)

Refrain

Mateso ya muda kitambo huku, tuyavumiliye, Muda kitambo Bwana atakuja, hatutayakumbuka.

Couplet 2

Neno lahubiriwa katika, Kanisa lake Bwana, Nasi tuwe tayari kutembea, Kama Neno lisemavyo (kweli)

Refrain

Mateso ya muda kitambo huku, tuyavumiliye, Muda kitambo Bwana atakuja, hatutayakumbuka.

Couplet 3

Tuwe hodari kwa Neno la Bwana, Tumpendeze Yeye, Ndipo tutashinda dunia na ya- liyomo ndani yake.

Refrain

Mateso ya muda kitambo huku, tuyavumiliye, Muda kitambo Bwana atakuja, hatutayakumbuka.

Couplet 4

Twapita katika zoruba nyingi, Na mawimbi humu, Lakini tumtegemeye Yesu, Tutashinda kwa Yeye.

Refrain

Mateso ya muda kitambo huku, tuyavumiliye, Muda kitambo Bwana atakuja, hatutayakumbuka.

Couplet 5

Walio safi mwendeleye mbele, Muwe safi sana, Yaliyo duniani yasituchoshe, Bali tuyashinde (yote).

Refrain

Mateso ya muda kitambo huku, tuyavumiliye, Muda kitambo Bwana atakuja, hatutayakumbuka.

Couplet 6

Tuheshimu wahubiri wachungaji, na wakristo wote Wandugu wote tuwapende sana, Pia tuwaombeye (kwa Bwana).

Refrain

Mateso ya muda kitambo huku, tuyavumiliye, Muda kitambo Bwana atakuja, hatutayakumbuka.

Couplet 7

Majaribu ni mema kwa wakristo, Wakiwa na imani, Nyuma ya jaribio kwao kweli, Wataona ushindi (wake).

Refrain

Mateso ya muda kitambo huku, tuyavumiliye, Muda kitambo Bwana atakuja, hatutayakumbuka.

Couplet 8

Lakini Bwana wetu Yesu Kristo, Ndiye ngao yetu, Hatuwezi kukosa lolote kwani, Yeye ana vyote (kweli).

Refrain

Mateso ya muda kitambo huku, tuyavumiliye, Muda kitambo Bwana atakuja, hatutayakumbuka.

Couplet 9

Tusiliyeliye kwa shida nyingi, Bali tumuombe Yeye, Pia tumtegemeye Mwokozi, Ndipo tutashinda (yote).

Refrain

Mateso ya muda kitambo huku, tuyavumiliye, Muda kitambo Bwana atakuja, hatutayakumbuka.

Couplet 10

Ndugu zangu sote tuwe hodari, Kwa Neno lake Bwana, Ndani ya hilo Neno ndipo sisi, Tutaweza kushinda (yote).