Indirimbo Zikundwa Open in the app

#341

Sauti nyingi zashawisha

Umuco 1

Refrain

[Trad. en Fr., voir Cant. n° 459]

Couplet 1

Sauti nyingi zashawisha, Duniani na fujo ni nyingi, Lakini siwezi kushindwa, Kutambuwa sauti ya Bwana.

Refrain

Yesu Mwokozi Anipenda, Ahadi zake ni za milele, Bwana-Arusi Akisema, Roho yangu inafarijika.

Couplet 2

Japo mabwana wawe wengi, Mimi ni wake Bwana Yesu, Ameninunuwa kwa damu, Mimi ni wake hata milele.

Refrain

Yesu Mwokozi Anipenda, Ahadi zake ni za milele, Bwana-Arusi Akisema, Roho yangu inafarijika.

Couplet 3

Mapumziko yalio bora, Ni kukaa miguuni kwake, Na kufundishwa siku zote, Mapenzi yake yaliyo kamili.

Refrain

Yesu Mwokozi Anipenda, Ahadi zake ni za milele, Bwana-Arusi Akisema, Roho yangu inafarijika.

Couplet 4

Sauti yake ni sahihi, Vingine vyote ni upuuzi, Yeye mkamilifu kweli, Akisema mimi naridhika.

Refrain

Yesu Mwokozi Anipenda, Ahadi zake ni za milele, Bwana-Arusi Akisema, Roho yangu inafarijika.

Couplet 5

Ndugu usipotoshwe sasa, Na upepo unavuma leo, Uje miguuni kwa Yesu, Utapata uzima wa milele.

Refrain

Yesu Mwokozi Anipenda, Ahadi zake ni za milele, Bwana-Arusi Akisema, Roho yangu inafarijika.

Couplet 6

Usimwitike yule Mwovu, A’kuonyesha dunia ya leo, fedha, dhahabu na ghasia, Ili wewe utupwe motoni.