Indirimbo Zikundwa Open in the app

#191

Safari ya kwenda mbinguni

Umuco 1

Couplet 1

Safari hiyi ya kwenda mbinguni, Ni ngumu sana, Bwana uniwezeshe, Kama sikuoni wewe Bwana wangu, Natetemeshwa na mambo ya huku.

Refrain

Ninasafiri kwa waliokombotewa, Ninasafiri huko juu mbinguni, {Oo Bwana wangu, Bwana wangu niokowe... Na giza hiyi ya mambo ya huku.} x2

Couplet 2

Safari hii ya kwenda mbinguni, Ni ngumu sana, Bwana unisaidie, Ona milima ni mirefu sana, Siwezi kitu Bwana uniwezeshe.

Refrain

Ninasafiri kwa waliokombotewa, Ninasafiri huko juu mbinguni, {Oo Bwana wangu, Bwana wangu niokowe... Na giza hiyi ya mambo ya huku.} x2

Couplet 3

Kwa nguvu zangu mimi siwezi kitu, Nakuhitaji, Bwana unitangulie, Nishike mkono niko juu ya bahari, Nishike mkono nisije kuzama.

Refrain

Ninasafiri kwa waliokombotewa, Ninasafiri huko juu mbinguni, {Oo Bwana wangu, Bwana wangu niokowe... Na giza hiyi ya mambo ya huku.} x2

Couplet 4

Wandugu zangu wamenitangulia, Kwa nguvu zako wameshinda yote, Na mimi Bwana niko mmoja wao, Nisaidie nifike Mbinguni.