Indirimbo Zikundwa Open in the app

#158

Mimi ni msafiri katika dunia

Umuco 1

Couplet 1

Mimi ni msafiri katika dunia, Ninasafiri katika safari, Ninaishi katika vita vya ajabu, Ninapigana na vita vya kila aina, Mimi ni msafiri na askari vitani.

Refrain

Jameni ninawezaje mimi, Kuwa msafiri kamili, Nisipojua hali za wasafiri? Jameni ninawezaje mimi, Kuwa askari kamili, Nisipopigana vita? Mimi ni msafiri na askari.

Couplet 2

Mimi ni msafiri katika dunia, Ninakutana na jaribu njiani, Ninakutana na masimba njiani, Ninapigana na kila jaribu, Mimi ni msafiri na askari vitani.

Refrain

Jameni ninawezaje mimi, Kuwa msafiri kamili, Nisipojua hali za wasafiri? Jameni ninawezaje mimi, Kuwa askari kamili, Nisipopigana vita? Mimi ni msafiri na askari.

Couplet 3

Mimi ni msafiri katika dunia, Nina ushindi katika safari, Njiani simba ninawashinda, Milima ninaipanda sana, Nina Mshindaji karibu nami.

Refrain

Jameni ninawezaje mimi, Kuwa msafiri kamili, Nisipojua hali za wasafiri? Jameni ninawezaje mimi, Kuwa askari kamili, Nisipopigana vita? Mimi ni msafiri na askari.

Couplet 4

Mimi ni msafjri katika dunia, Jaribu linanipa kuwa macho, Linanipa kuamka na kujijuwa, Jaribu linanipa kujiadhari sana, Jaribu linanipa kuwa na ufahamu.

Refrain

Jameni ninawezaje mimi, Kuwa msafiri kamili, Nisipojua hali za wasafiri? Jameni ninawezaje mimi, Kuwa askari kamili, Nisipopigana vita? Mimi ni msafiri na askari.

Couplet 5

Mara ninapokutana na jaribu, Ndipo ninaamka uzimani mwangu, Kama sijaribiwi ninajisahau, Lakini sasa silali vitani, Mimi ninapigana vita vizuri sana.