#96
Mbingu za mbingu zimefunguliwa
Umuco 1
Couplet 1
Mbingu za mbingu zimefunguliwa, Kwa ajili yako mwaminifu, Uliempokea Bwana Yesu, Milango yote iko wazi, Kwa wale waliomwamini, Karibu uingie uzimani.
Refrain
{Njoo mwaminifu uingie katika lango hilo, lango limefunguliwa, Bwana Yesu amelifungua.} x2
Couplet 2
Milango yote imefungwa, kwa wale wasiomwamini, Wanangojea kuteketezwa, Kila kazi ya mtu itapimwa, Waruka-ukuta watapimwa, Matendo yote yatapimwa.
Refrain
{Njoo mwaminifu uingie katika lango hilo, lango limefunguliwa, Bwana Yesu amelifungua.} x2
Couplet 3
Mtu mwenye kujipendekeza, Na mambo ya kukufuru, Huyo sio mwana wa ufalme, Watoto wa Kora na Balamu, wajaana kiburi, majivuno, Hawapiti katika lango.
Refrain
{Njoo mwaminifu uingie katika lango hilo, lango limefunguliwa, Bwana Yesu amelifungua.} x2
Couplet 4
Mlango sasa uko wazi, kwa wale wanaouona, Wanaojua Mwokozi wao, Vizuri vyajaana umwo, vilivyoandaliwa wote, Wanaopita mlangoni.
Refrain
{Njoo mwaminifu uingie katika lango hilo, lango limefunguliwa, Bwana Yesu amelifungua.} x2