#157
Kijito cha utakaso
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Kijito cha utakaso ni damu ya Yesu, Bwana anao uwezo kunipa Wokovu.
Refrain
Kijito cha utakaso, Nizame kuoshwa humo Namsifu Bwana kwa hiyo Nimepata utakaso.
Couplet 2
Viumbe vipya naona; damu ina nguvu, imeharibu uovu ulionidhulumu.
Refrain
Kijito cha utakaso, Nizame kuoshwa humo Namsifu Bwana kwa hiyo Nimepata utakaso.
Couplet 3
Naondoka kutembea nuruni mwa Mbingu, Na moyo safi kabisa kumpendeza Mungu.
Refrain
Kijito cha utakaso, Nizame kuoshwa humo Namsifu Bwana kwa hiyo Nimepata utakaso.
Couplet 4
Ni neema ya ajabu kupakwa na damu; na Bwana Yesu kumjua Yesu wa Msalaba.