Indirimbo Zikundwa Open in the app

#156

Bwana Yesu yuko wapi

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Bwana Yesu yuko wapi, Mpenzi wangu rafiki? Njia gani amekwenda? Nitamwonaje mimi? Roho yangu yajutishwa Na dhambi na huzuni; Yesu mpenzi wangu Mwema Namtafuta kwa bidii.

Couplet 2

Ninapaza sauti yangu Nalia:wapi Yesu? Ndani mwangu sina raha Mpaka nimwone Yesu. Ningekuwa na mabawa Ningeruka upesi Milimani, mabondeni Kumtafuta Bwanangu.

Couplet 3

Aondoa shida zangu, Maharibifu yote. Nikiona taabu mimi Anituliza yeye. Nitafanya bidii sana; Kumtafuta popote; Sitachoka kutembea Mchana hata usiku.

Couplet 4

Bwana Yesu nitokee, Roho inakuita. Niondoe na maovu Yesu Mwokozi wangu. Utilize hamu yangu Kaa kwangu daima. Nikupende sana wewe, Niwe wako milele.