Indirimbo Zikundwa Open in the app

#152

Uliyesulubishwa

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Uliyesulubishwa, Mtakatifu Bwanangu, Uwe ngao shidani, uniombee mimi. Uliyesulubishwa, Mtakatifu Bwanangu!

Couplet 2

Wongofu sina hata, niondolee makosa. Mwovu akinishtaki nasumbuka rohoni. Wongofu sina hata, niondolee makosa.

Couplet 3

Wewe tu nipokee, nakukumbilia wee. Hata nifanye bidii, nikatoe machozi. Wewe tu nipokee, nakukimbilia wewe.

Couplet 4

Uwe ngao shidani, Niombee na mimi! Hapa nikiumizwa, Saa ya mwisho ikija: Uwe ngao shidani, Niombee na mimi!