#150
Haya ee moyo wangu
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Haya ee moyo wangu, imba kwa furaha. Umwimbie Muumbaji Mbingu na dunia. Atukuzwaye pote umsifu na wewe kwa nguvu zako zote, umri wako wote.
Couplet 2
Mungu wake Yakobo. ndiye Mungu wwetu. Ukimchagua yeye, una fungu jema, unacho kitu chema, umepata mali; moyo utakung’aa shida zitakwisha.
Couplet 3
Ni mwenye nguvu nyingi, hana amshindaye, kwa hekima aumba vyote ni ajabu, misitu na mabonde, milima, mashamba, vilivyo baharini wanyama porini.
Couplet 4
Ana mizungu mingi, kuponya wanawe. Anawapa riziki, hata siku za njaa. Wenye chakula haba wanenepa miili: hata waliofungwa anawafungua.
Couplet 5
Mashangilio yote hayamtoshi yeye. Ni mwema peke yake nami ni vumbi tu! Ananihurumia kwa kuwa ni wake, kwa hiyo nalikuza Jina lake pote.