#149
Haya, umati wa Yesu
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Haya, umati wa Yesu, Ulioungwa naye! Haya, enendeni hima Katika vita kubwa! Shetani tayari, Kupigana na sisi!
Couplet 2
Tumfuate Yesu Kristo, Tumwamini yeye tu. Mwovu akituvizia Sisi hatuogopi. Majeshi ya Mbingu Ni pamoja na sisi!
Couplet 3
Tukikesha na kuomba Yesu anayotaka, Tukishika neno lake Na kumtegemea Kwa nguvu hizi tu Tutaweza kushinda!
Couplet 4
Sasa haya wenzi wangu, Tumfuate Yesu tu! Siku za maisha yetu, Tuwe katika yeye. Tuache dunia Kuingia Mbinguni!
Couplet 5
Pale Mungu atawapa Taji walioshinda, Wapate urithi wao Nyumbani mwa milele. Hayani! Tuimbe, Tumsifu Bwana wetu!