#146
Neno la Mungu takata
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Neno la Mungu takata Lililotoka Mbinguni; Ambalo moto na panga Haziwezi kulishinda.
Refrain
{Twakushika siku zote Maishani na kufani.} x2
Couplet 2
Waliotutangulia Waliokutegemea, Wamekufia mashujaa; Nasi tulio watoto.
Refrain
{Twakushika siku zote Maishani na kufani.} x2
Couplet 3
Neno la Mungu takata, Tukushuhudie nasi Kwa neno tamu na tendo Kunako wenzi au adui.
Refrain
{Twakushika siku zote Maishani na kufani.} x2