Indirimbo Zikundwa Open in the app

#147

Tegemea mpaka kufa

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Tegemea mpaka kufa, Utapata Wokovu. Bwana Yesu ni Mwokozi Yeye anakupenda. Uje kwake ‘sikawie’. Yeye akuokoa.

Refrain

Njoo upesi! Njoo upesi! Fika kwa Bwana Yesu.

Couplet 2

Acha mambo ya dunia Yakuhangaishayo. Iko mali ya uzima Unaitiwaa hiyo. Mali hiyo ni uzima Utapewa na Bwana.

Refrain

Njoo upesi! Njoo upesi! Fika kwa Bwana Yesu.

Couplet 3

Wakatae, waepuke Wanaokudanganya; Na wajinga, wakuponza, Wakupoteza wewe. Ila wewe ukatae Kuondoka kwa Yesu.

Refrain

Njoo upesi! Njoo upesi! Fika kwa Bwana Yesu.

Couplet 4

Ukijua jambo hilo Usipolifuata Kosa hilo kubwa sana, Wapasiwa hukumu. Vumilia, jizuie Utapata uzima.

Refrain

Njoo upesi! Njoo upesi! Fika kwa Bwana Yesu.

Couplet 5

Bwana Yesu amekwisha Kukutengenezea Kitu chema kwake Mungu, Ndiko unakokwenda. Kile kitu upendacho Kule utakipewa.

Refrain

Njoo upesi! Njoo upesi! Fika kwa Bwana Yesu.