#145
Ndoa yetu nzima simika
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Ndoa yetu nzima simika, Yesu! Usiku na mchana uwepo kwetu. Leo tuna raha, Wewe watupa.
Refrain
Ndoa yetu Bwana ndiwe Baraka!
Couplet 2
Atoka kijana, ataka mchumba siku zinapita za kupimana. Leo twapatana pamoja kukaa
Refrain
Ndoa yetu Bwana ndiwe Baraka!
Couplet 3
Vyote hapa chini vinakaa muda, vyote vinaoza, tena vyachakaa. Pendo la duniani nalo huchakaa.
Refrain
Ndoa yetu Bwana ndiwe Baraka!
Couplet 4
Kakaa kwetu Bwana, kutukagua, pendo letu sisi lisichakae: Hivi na tukae na baraka tu.
Refrain
Ndoa yetu Bwana ndiwe Baraka!
Couplet 5
Kana arusuni ulialikwa, walivyoishiwa ukaongeza, nasi shida zetu utazishinda.
Refrain
Ndoa yetu Bwana ndiwe Baraka!