#144
Mbele ninaendelea
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Mbele ninaendelea, ninazidi kutembea. Maombi uyasikie, Ee Bwana, unipandishe.
Refrain
Ee, Bwana, uniinue, Kwa imani nisimame; Nipande milima yote, Ee Bwana, Unipandishe.
Couplet 2
Sina tamani nikae, Mahali pa shaka, kamwe; Hapo wengi wanakaa, Kuendelea naomba.
Refrain
Ee, Bwana, uniinue, Kwa imani nisimame; Nipande milima yote, Ee Bwana, Unipandishe.
Couplet 3
Nisikae duniani, asumbuapo Shetani; Natazamia Mbinguni, nitafika na imani.
Refrain
Ee, Bwana, uniinue, Kwa imani nisimame; Nipande milima yote, Ee Bwana, Unipandishe.
Couplet 4
Nataka nipandishwe juu, Zaidi yale mawingu. Nitaomba nifikishwe, Ee Bwana unipandishe.