Indirimbo Zikundwa Open in the app

#141

Pana jito, lina Maji mazuri

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Pana jito, lina Maji mazuri, Yaenda ulimwenguni. Lametameta nalo Linang’aa. Walijua jito hilo?

Refrain

Ninakuita nawe njoo! Utafute jito hilo! Maji yake yapoza Moyo. Nawe yateke unywe.

Couplet 2

Wanywao maji haya wafurahi, waimba kwa shangwe kubwa. Makosa na shida Yanaondoshwa, Wote waoshwa na Bwana.

Refrain

Ninakuita nawe njoo! Utafute jito hilo! Maji yake yapoza Moyo. Nawe yateke unywe.

Couplet 3

Jito hilo latoa maji mengi, matamu yapendezayo. Yaponya wagonjwa, Yatia nguvu, Uchafu watakashika.

Refrain

Ninakuita nawe njoo! Utafute jito hilo! Maji yake yapoza Moyo. Nawe yateke unywe.

Couplet 4

Maji ya jito hilo ni uzima unaotoka Kwa Yesu. Damu yake yenye kiasi kikuu Imemwagwa tusafike.

Refrain

Ninakuita nawe njoo! Utafute jito hilo! Maji yake yapoza Moyo. Nawe yateke unywe.