Indirimbo Zikundwa Open in the app

#136

Msifuni, Yesu ndiye Mkombozi

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Msifuni, Yesu ndiye Mkombozi; Imbeni ya pendo zake kuu, Sujuduni, malaika mlioko, Jina lake liwe na sifa kuu. Kama vile Mchunga uchungavyo Vivyo sisi kutwa atachunga. Msifuni mlio wake watoto Msifuni aliye Mchunga.

Couplet 2

Msifuni, Yesu ndiye mkombozi; Akateswa tupate ongoka; Ndiye Mwamba, Dhamana ya kuokoka; Sujuduni kwake muangikwa, Yesu aliyeudhiwa na hamu Kwa pendo za baba yake Mungu. Aliyefyolewa na kusulubiwa. Msifuni ndilo letu fungu.

Couplet 3

Msifuni, Yesu ndiye Mkombozi; Shindukeni, enyi malango juu; Bwana Yesu tangu milele Mwokozi, Mvikeni taji, ni yake tu. Atakuja kuitawala nchi, Yesu, Mwombezi wetu wa Mungu. Msifuni, ni mfalme wa salama; Ndiye kweli mwana wake Mungu.