Indirimbo Zikundwa Open in the app

#135

Mapenzi ya milele

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Mapenzi ya milele Ndiyo yanipendezayo; Yalinipenda mbele, Sina fahamu nayo; Sasa amani yake Tele rohoni mwangu, Ni mimi kwa kuwa wake, Na yeye kuwa wangu, Ni mimi kuwa wake, Na yeye kuwa wangu

Couplet 2

Mbingu zinang’ara juu, Na nchi nayo vivyo; Macho ya dunia tu Hayajaona hivyo; Nyuni huimba sana, Maua yana rangi, Ni kumjua Bwana Na pendo zake nyingi, Ni kumjua Bwana Na pendo zake nyingi,

Couplet 3

Mambo mengi maovu Nayo yenye kutisha, Sasa hayana nguvu, Si yenye kututisha; Ni mkononi mwake, Nalindwa salamani Ninajua ni wake, Ni wake mapenzini. Ninajua ni wake, Ni wake mapenzini.

Couplet 4

Wake hata milele, Si kutengana tena; Hunipa raha tele Moyoni mwangu, Bwana; Hiyo nchi na Mbingu Zitatoweka zile, Ni wake, Yeye wangu, Milele na milele. Ni wake, Yeye wangu, Milele na milele.