Indirimbo Zikundwa Open in the app

#137

Yesu Mponya

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Yesu ndiye Mganga wetu Aponya wagonjwa wote; Mganga wetu ni Yesu, Aponyaye hasira.

Refrain

Tumsifu huyo Yesu Tumsifu milele, Kwani Mponya mtakata Mwokozi wa wanyonge.

Couplet 2

Mganga wetu ni Yesu Huondoa matusi; Mganga wetu ni Yesu, Mwenye kuponya choyo.

Refrain

Tumsifu huyo Yesu Tumsifu milele, Kwani Mponya mtakata Mwokozi wa wanyonge.

Couplet 3

Mganga wetu ni Yesu Huponya wivu wetu; Yesu ndiye aponyae Kelele za nyumbani.

Refrain

Tumsifu huyo Yesu Tumsifu milele, Kwani Mponya mtakata Mwokozi wa wanyonge.

Couplet 4

Mganga wetu ni Yesu Mponya wa tamaa mbaya; Mganga wetu ni Yesu Uasherati hufuta

Refrain

Tumsifu huyo Yesu Tumsifu milele, Kwani Mponya mtakata Mwokozi wa wanyonge.

Couplet 5

Mganga wetu ni Yesu Aponya kiu cha pombe, Mganga wetu ni Yesu Kila dhambi uponya.