#134
Juu yake langu shaka
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Juu yake langu shaka, Yesu namuwekea, Nami sitafedheheka Nikimtegemea.
Refrain
Natumai, natumai, Nnatumai kwake tu; Natumai, natumai, Natumai kwake tu.
Couplet 2
Juu yake, dhambi zangu; Aniosha kwa damu; Nionekane kwa Mungu, Nisiye na laumu.
Refrain
Natumai, natumai, Nnatumai kwake tu; Natumai, natumai, Natumai kwake tu.
Couplet 3
Juu yake yangu hofu; Kwake nimetulia; Sipotei kwa upofu Njia aning’azia.
Refrain
Natumai, natumai, Nnatumai kwake tu; Natumai, natumai, Natumai kwake tu.
Couplet 4
Juu yake raha yangu; Humuangalia tu; Mwenye kila ulimwengu, Aniruzuku na huu.
Refrain
Natumai, natumai, Nnatumai kwake tu; Natumai, natumai, Natumai kwake tu.
Couplet 5
Juu yake, moyo wangu; Hali yangu na mali; Mimi wake, Yeye wangu, Twapasana kamili.