#133
Ni wako Mungu
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Ni wako Mungu! Ni furaha kwangu, Ni raha kumjua Mwokozi wangu.
Refrain
Aleluya enzi ndako; Aleluya, Amin. Aleluya, enzi ndako; Rejea Yesu.
Couplet 2
Mwana wa Mungu Ndiye fungu langu, Na moyo hufurahi kwa Yesu wangu.
Refrain
Aleluya enzi ndako; Aleluya, Amin. Aleluya, enzi ndako; Rejea Yesu.
Couplet 3
Raha ya kweli Ina jina hili, Na aliyeshika, ana Mbingu kweli.
Refrain
Aleluya enzi ndako; Aleluya, Amin. Aleluya, enzi ndako; Rejea Yesu.
Couplet 4
Nimeingia Mapendano haya, Nimepata uzima na Mbingu pia.
Refrain
Aleluya enzi ndako; Aleluya, Amin. Aleluya, enzi ndako; Rejea Yesu.
Couplet 5
Nilipo chini, Ni mwako kazini Hata nije kwako uliko Mbinguni.