Indirimbo Zikundwa Open in the app

#132

Sauti sikilizeni

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Sauti sikilizeni Za waimbao juu, “Aleluya, Aleluya, Aleluya, mkuu!” Wako makundi-makundi Kama nyota wang’ara, Kwa makuti ya mitende, Na meupe wamevaa.

Couplet 2

Wazazi na manabii Wafanyaji wa njia; Mashahidi, waandishi, Nao wafalme pia! Mabikira kina-mama, Wajane wa kusali, Waimba wakikutana “Msifunu Imanweli”.

Couplet 3

Watu toka huzunini Wameosha na nguo, Ni kwa damu yake Yesu; Maonjo, mbali nao! Walitekwa, walikatwa Hata kwa misumeno, Kwao kifo na Shetani Walishindiwa mno.

Couplet 4

Mungu mumo mwake Mungu, Nuru mumu mwa nuru, Kwa kufungamana mwako Tutaishi mahuru; Tujalize, Imanweli, Kujaa kwako wewe Mungu Baba, Mungu Mwana, Mungu Roho, tunawe.