Indirimbo Zikundwa Open in the app

#125

Ati twonane Mtoni?

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Ati twonane mtoni? Maji mazuri ya Mbingu; Yanatokea mwangani, Penye kiti cha Mungu.

Refrain

Naam, twonane mtoni! Watakatifu, kwenu ni mtoni! Tutakutanika mtoni Penye kiti cha Mungu.

Couplet 2

Tukitembea mtoni Na Yesu Mchunga wetu Daima tu ibadani Usoni pake kwetu.

Refrain

Naam, twonane mtoni! Watakatifu, kwenu ni mtoni! Tutakutanika mtoni Penye kiti cha Mungu.

Couplet 3

Kwang’ara sana mtoni Cha Mwokozi ni kioo, Milele hatuachani, Tumsifu kwa nyimbo.

Refrain

Naam, twonane mtoni! Watakatifu, kwenu ni mtoni! Tutakutanika mtoni Penye kiti cha Mungu.

Couplet 4

Si mbali sana mtoni, Karibu tutawasili, Mara huwa furahani Na amani ya kweli.