#124
Mungu ulisema
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Mungu ulisema, Giza ilikoma; Twakushukuru! Twakusihi sote, Duniani mote Na kwa watu wote, Iwe nuru.
Couplet 2
Yesu ulikuja, Ulituletea Nuru kuu; Macho kwa vipofu, Maisha kwa wafu; Twakushukuru.
Couplet 3
Roho kiongozi, Roho wa mapenzi Tia nuru; Mwovu hata sasa Watu huwatosa, Tunakwomba hasa, Iwe nuru.
Couplet 4
Mungu wa utatu Mwanga wao watu, Tuwe huru; Twende kote-kote Wafundishwe wote, Duniani mote, Iwe nuru.