#126
Ni Mji mzuri
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Ni mji mzuri, Mbali sana; Watu wanawiri Kama jua; Waimba kwa tamu, Tuna wema hakimu: Sifa na idumu, Kwake Bwana.
Couplet 2
Ni mji mzuri Twende sote! Una na fahari Msikawe! Raha tutaona, Dhambi hapana tena; Hatutaachana Siku zote.
Couplet 3
Ni mji mzuri; Macho yote Huko wanawiri Kama pete; Baba tutamwona, Tukifanywa tu wana; Tumo kupendana Naye sote.
Couplet 4
Ni mji mzuri; Tusipotee Na tuwe hodari, Tuupate! Tufunze, tutume Kwa taji na ufalme: Sifa na zivume Siku zote.