Indirimbo Zikundwa Open in the app

#123

Nimeketi mini nili kipofu

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Nimeketi mimi nili kipofu Gizani nangojea macho; Ewe Bwana Yesu mwenye Wokovu, Ondoa dhambi zangu nzito.

Refrain

Huruma hakuna aonaye, Gizani nagojea macho, Sasa nitakase nikusihiye, Yesu, na dhambi zangu nzito.

Couplet 2

Tangu siku nyingi nimepofuka Natamani uso nikwone; Ewe Bwana Yesu, mwenye baraka Sema neno, basi, nipone.

Refrain

Huruma hakuna aonaye, Gizani nagojea macho, Sasa nitakase nikusihiye, Yesu, na dhambi zangu nzito.

Couplet 3

Nimeketi mimi nili na giza, Nami ya kutumai sina; Ili nasikia kunong’oneza, “Kwake Yesu kuna kupona.”

Refrain

Huruma hakuna aonaye, Gizani nagojea macho, Sasa nitakase nikusihiye, Yesu, na dhambi zangu nzito.