Indirimbo Zikundwa Open in the app

#122

Bwana Yesu

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unaumia? Unateseka sana, Kwa ajili ya kuomba, Waomba na jasho jingi likageuka damu.

Refrain

Kumbe! Ni dhambi zangu zinazokuumiza. Bwana wangu, Mungu wangu, mimi leo, naja kwako ili niziungame.

Couplet 2

Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unaumia, na mizigo mizito? Umejitwalia wewe, Msalaba mabegani Kwa ajili ya watu.

Refrain

Kumbe! Ni dhambi zangu zinazokuumiza. Bwana wangu, Mungu wangu, mimi leo, naja kwako ili niziungame.

Couplet 3

Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unatukanwa, wawambwa kama mwizi, Bila kosa ukalia, Baba yangu, wasamehe, Chukua roho yangu.

Refrain

Kumbe! Ni dhambi zangu zinazokuumiza. Bwana wangu, Mungu wangu, mimi leo, naja kwako ili niziungame.

Couplet 4

Bwana Yesu, Bwana Yesu, Muda ulipofika, nchi ikawa giza, Mbinguni pakatulia, Angani pakawa kimya, Watu wakaogopa.

Refrain

Kumbe! Ni dhambi zangu zinazokuumiza. Bwana wangu, Mungu wangu, mimi leo, naja kwako ili niziungame.

Couplet 5

Bwana Yesu, Bwana Yesu, Jinsi ulivyoumwa, ukamwomba Baba, Leo umeshinda kifo, sasa wapaa Mbinguni, Naimba, Haleluya.