#121
Liko lango moja wazi
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Liko lango moja wazi, Ni lango la Mbinguni; Na wote waingiao Watapata nafasi.
Refrain
Lango ndiye Yesu Bwana Wote waingie kwake, Lango! Lango La Mbinguni ni wazi.
Couplet 2
Yesu ndiye lango hili, Hata sasa ni wazi, Kwa wakubwa na wadogo, Tajiri na maskini.
Refrain
Lango ndiye Yesu Bwana Wote waingie kwake, Lango! Lango La Mbinguni ni wazi.
Couplet 3
Hili ni lango la raha, Ni lango la rehema; Kila mtu apitaye Hana majonzi tena.
Refrain
Lango ndiye Yesu Bwana Wote waingie kwake, Lango! Lango La Mbinguni ni wazi.
Couplet 4
Tukipita lango hili Tutatua mizigo, Tuliochukua kwanza, Tutavikwa uzima.
Refrain
Lango ndiye Yesu Bwana Wote waingie kwake, Lango! Lango La Mbinguni ni wazi.
Couplet 5
Hima ndugu tuingie Lango halijafungwa, Likifungwa mara moja Halitafunguliwa.