Indirimbo Zikundwa Open in the app

#120

Enyi wanadamu

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Enyi wanadamu mbona Sana mwatanga-tanga, Kama kondoo wanyonge, Wasio na Mchunga? Yuko Mchunga mmoja Mwenye mapenzi mema; Haya kutaneni kwake, Atawachunga vyema.

Couplet 2

Mungu tunamwona kuwa Mwenye uwezo wote; Na nguvu zake zapita Mawazo yetu yote: Ni Baba, mapenzi yake Ni makubwa hakika; Hatuwezi kuyajua, Na hayana mpaka.

Couplet 3

Rehema za Mungu nazo Zina upana sana; Kama huo wa bahari, Mwisho wake hapana; Haki yake ina mema, Kwa hayo twashukuru, Kwetu uko msamaha, Furaha na uhuru.

Couplet 4

Mapenzi yake mapana, Sisi hatuna cheo Cha kutosha, nao moyo Una wema upeo; Ukombozi mwingi mno Katika damu yake; Sote twapata furaha, Kwa maumivu yake.

Couplet 5

Yesu mkaribieni Njoni msife myoyo; Njoni kwake kwa imani, Mema yake ni hayo; Heri tuwe kama wana Tushike neno lake, Daima atujaza Tele furaha yake.