Indirimbo Zikundwa Open in the app

#119

Si damu ya nyama

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Si damu ya nyama Iliyomwagika Iwezayo kuondoa Dhambi za wakosa.

Couplet 2

Yeye Bwana Yesu Sadaka ya Mungu, Mwenye damu ya thamani, Ni Mwokozi kweli.

Couplet 3

Kwa imani yangu, Namshika yeye, Naziweka dhambi zangu Juu ya kichwa chake.

Couplet 4

Mzigo wa dhambi Sichukui tena, Ameuchukua yeye, Juu ya Msalaba.

Couplet 5

Bwana Yesu ndiye, Mwokozi wa kweli Tumsifu siku zote, Twapata uhuru.