Indirimbo Zikundwa Open in the app

#118

Ni Ujumbe wa Bwana

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Ni Ujumbe wa Bwana, Aleluya! wa maisha ya daima, Amenena mwenyewe, Aleluya! Utaishi ukitazama.

Refrain

Tazama, ishi sasa! Kumtazama Yesu, Amenena mwenyewe, Aleluya! Utaishi ukitazama.

Couplet 2

Ni ujumbe wa wema, Aleluya! Nawe shika, rafiki yangu! Ni habari ya raha Aleluya! Mwenye kuinena ni Mungu.

Refrain

Tazama, ishi sasa! Kumtazama Yesu, Amenena mwenyewe, Aleluya! Utaishi ukitazama.

Couplet 3

Uzima wa daima, Aleluya ! Kwake Yesu utauona. ukimtazama tu, Aleluya! Wokovu u pweke kwa Bwana.

Refrain

Tazama, ishi sasa! Kumtazama Yesu, Amenena mwenyewe, Aleluya! Utaishi ukitazama.