#117
Tufani inapovuma
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Tufani inapovuma Sana moyoni mwangu, Huona pa kujificha Mkononi mwa Mungu.
Refrain
Hunificha, hunificha Adui hatanipata, Hunificha, hunificha, Mkononi mwake.
Couplet 2
Pengine kuna taabu Yanisongeza kwake; Naijua si hasira, Ni ya mapenzi yake.
Refrain
Hunificha, hunificha Adui hatanipata, Hunificha, hunificha, Mkononi mwake.
Couplet 3
Adui wakiniudhi Nami nikisumbuka, Mungu atavigeuza Vyote viwe baraka.
Refrain
Hunificha, hunificha Adui hatanipata, Hunificha, hunificha, Mkononi mwake.
Couplet 4
Niishipo duniani Ni tufani daima, Anilindapo rohoni Nitakaa salama.