#116
Bwana, U sehemu yangu
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Bwana U sehemu yangu, Rafiki yangu wewe; Katika safari yangu Tatembea na wewe; Pamoja na wewe, Pamoja na wewe, Katika safari yangu Tatembea na wewe.
Couplet 2
Mali hapa sikutaka, Ili niheshimiwe, Na yanikute mashaka Sawa sawa na wewe, Pamoja na wewe, Pamoja na wewe, Heri nikute mashaka Sawasawa na wewe.
Couplet 3
Niongoze safarini, Mbele unichukue Mlangoni kwa Mbinguni Niingie na wewe. Pamoja na wewe, Pamoja na wewe, Mlangoni kwa Mbinguni, Niingie na wewe.