Indirimbo Zikundwa Open in the app

#115

Kilima kando ya Mji

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Kilima kando ya mji Alikufa Bwana; Kuokoa wakosaji Akateswa sana.

Couplet 2

Kabisa hayasemeki, Mateso dhaifu Alikufa mwenye Haki Tupate Wokovu.

Couplet 3

Alimwaga damu yake Ili tuwe wema, Tufae kukaa kwake Mbinguni daima.

Couplet 4

Hatuna mwenye imani Aliye na haki, Wa kutosha yetu deni, Rafiki Yesu tu.

Couplet 5

Alijua peke yake Kufungu Mbingu Ufunguo damu yake Kondoo wa Mungu.

Couplet 6

Aliyetupenda hivyo Nasi tumpende, Tukamtumai vivyo Na kazi tutende.