Indirimbo Zikundwa Open in the app

#112

Nilikupa wewe Maisha yangu

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Nilikupa wewe Damu ya moyoni, Ili wokolewe, Winuke ufuni: Nimekunyimani? Umenipa nini?

Couplet 2

Nilikupa miaka Yangu duniani Upate inuka, Kuishi Mbinguni: Nimekunyimani? Umenipa nini:

Couplet 3

Niliacha nuru Za Baba, Mbinguni, Kwingia taabu Za ulimwenguni: Nimekunyimani? Umenipa nini?

Couplet 4

Niliteswa sana, Mateso kifoni, Usije yaona Hayo ya motoni: Nimekunyimani? Umenipa nini?

Couplet 5

Nimekuletea Huku duniani Upendo na afya Zatoka Mbinguni: Nimekunyimani? Umenipa nini?

Couplet 6

Nipe siku zako, Udumu mwangani; Na taabu yako, Wingie rahani Nafsi, pendo, mali, Twae Imanweli.